Floyd Mayweather na Manny Pacquiao wawashiana moto


Mabondia wawili ambao wamekuwa wakifanya vizuri miaka ya hivi karibuni Floyd Mayweather na Manny Pacquiao, wameonesha kutofautiana huku kila mmoja akivimba juu ya mwenzake.

Tofauti hizo wamezionesha kupitia mitandao ya kijamii, baada ya Mayweather kulalamika kuwa kila Pacquiao anapokuwa anafanya jambo lake lazima jina lake litajwe, kitu ambacho amedai ni kumpa umaarufu bondia huyo raia wa Ufilipino.

''Nashangaa huyu mtu hawezi kusimama peke yake mpaka jina langu litajwe ili kitu chake kifahamike, mara watake nirudiane naye wakati nimeshamchapa vya kutosha, nina hela kuliko yeye na ninamzidi kwenye kila jambo nikiwa na rekodi ya kutopoteza pambano'', aliandika Mayweather.

Kwa upande wake Pacquiao amemjibu Floyd kwa kumwambia kuwa yeye kabla ya kuelezea jambo lake kwenye mitandao ya kijamii, ametumia jina la Pacquiao  hivyo inaonesha jinsi gani yeye ndio anataka mteremko.

Pacquiao na Mayweather walikutana Mei 2, 2015 ambapo Floyd Mayweather aliibuka mshindi kwa pointi ambapo majaji watatu walitoa pointi hizi 118–110, 116–112, 116–112.

Ugomvi huu wa kwenye mitandao unatafsiriwa kama kichocheo cha wawili hao kurejea ulingoni, kitu ambacho kimekuwa kikisubiriwa kwa hamu na wapenzi wa ngumi duniani.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad