FOREX TRADING TANZANIA | Yafahamu Haya Kabla ya kujiingiza Kwenye Hii Biashara.

Habari. Ndugu waTanzania Mimi nikiwa kama mdau na miongoni Mwa Wa Tanzania wachache Walio wahi kuanza na kuyaona Mafanikio ya hii sekta mpya hapa nchini ya Forex trading, leo hii nimeona kuna ulazima wa kuandika Makala hii ili kumsaidia Mtazania yoyote popote alipo anayetamani kufanya hii biashara. Waweza jiuliza kwa nini nachukua jukumu hili? Mafanikio katika sekta hii sio rahisi kama inavyo onekana kwenye mitandao yakijamii na haswa kwa jinsi Forex Trading Tanzania ilivyo letwa, safari yangu ya mafanikio haikua rahisi, ilikua ni safari ya maumuvi makali ya kupoteza pesa yalio nilipelekea matatizo chungu nzima ambayo haina maana ya kuyaweka hapa. 
Hivyo basi nimeona nifanye hivi kama njia moja wapo yakurudisha au kutoa kwa jamii bure kabisa kumsaidia yule anayeanza au ambae yupo safarini kuelekea mafanikio kwenye hii sekta, ili kuepukana na matatizo makubwa niliyo yapitia na kumsaidia kuyaona mafanikio kwa urahisi Zaidi.
Kama ningekua na mashine ya kurudisha muda nyuma, niwe mimi yule mgeni wa forex trading miaka miwili  iliyopita, ningefanya hivyo ili tuu niwe na haya ninayo yafahamu leo kwa hakika ingenirahisisha  nakuongeza spidi ya mafanikio yangu na ningeyapata kwa haraka Zaidi. Lakini kibaya ni kwamba hakuna mashine kama hiyo lakini kwa wewe unaenza sasa, hii nikama lulu kwako hivyo basi hivi ndo vitu vitano ambavyo ningevijua mwanzoni naamini  kwa asilimia mia moja ningefanikiwa mapema Zaidi.

MATUMIZI YA INDICATORS NI UPOTEVU WA MUDA

Hiki ni kitu ambacho kingeniokoa na upotevu wa muda na kuumiza kichwa, kama ningefahamu mapema kuwa indicators ni upotevu wa muda ingepunguza mahangaiko yakujifunza. Sasa hii ni fursa ya wewe kuepukana na hiki kitu, najua mwanzoni zinaweza zikaonekana kama ni ujanja pale ukionesha marafiki na jamaa platform yako imejaa mistari mingi ya indicators lakini nakuhakikishia ni sawa nakujichimbia kaburi hatua kwa hatua jinsi kila siku unavyoendelea kuzitumia.
Kama umengundua mpaka sasa indicators zimetokana na Mjumuiko wa vigezo vya PRICE ACTION  hivyo basi kwanini uzitumie wakati unaweza tumia price action moja wa kwa moja.. Mafaniko kwenye hii sekta yanatokana na kuweka mambo kiurahisi yaani kupunguza vigezo vingi vinavyofanya ufanye maamuzi ya kununua na kuuza na sio vinginevyo. Mafaniko yangu yalianza kuoneka pale nilipo anza kutumia PRICE ACTION.
Kweli kabisa ‘moving averages’ zinausaidizi haswa kwa wageni na hii biashara kungundua ‘Support na resistance levels’ na Trend, ukweli ni kwamba kutoa Moving averages sioni umuhimu wa kutumia indicators na ahata hizi Moving averages zisitumii kabisa skuizi ni natumia PURE PRICE ACTION maana nimeshajenga uzoefu wa hali ya juu.
NI RAHISI KU OVERTRADE KULIKO UNAVYO FIKIRIA.
Kitu ambacho niligundua baada ya kuwa mzoefu kwenye biashara hii siku za mwanzoni nilikua na overtrade na hata siku gundua na fanya hilo.
Nirahisi kutafuta visingizio vya trades unazochukua kwa wingi (kwaku overtrade). Lakini jibu kamili nikwamba je ime timiza vigezo vyako vya kutrade yaani (strategy)
Overtading nikitendo cha kuchukua trade nje ya strategy yako na niamini mimi, sio jambo gumu sana kufanya kwenye hii biashara, haswa kwa Traders wageni na nijambo ambalo lina umiza sana na kurudisha nyuma hatua zako zakimafanikio.
MATUMIZI YA TIMEFRAME NDOGO NI HATARI
Ukiangalia kwa makini hizi points zote zinaingiliana kwa mfano overtrading inasababishwa nakuangalia timeframe ndogo kama zile chini ya ‘1HOUR’,  laiti kama ningerudi nyuma kipindi nikiwa mgeni na forex ningejieleza haswaa  umuhimu wa matumizi ya timeframe za juu. Matumizi ya timeframe za chini yatakupelekea kuovertrade kwa sababu utahisi unaona fursa nyingi sokoni wakati kiukweli izo ni kele tu za soko. Kirahisi ni kwamba fursa zinazo patika timeframe za juu zina Asimilia kubwaa Zaidi ya kukutengenezea faida kuliko zile zinazo patikana timeframe za chini.
Endelea Kujifunza kwa undani Biashara hii kwenye platform Yetu kupitia Tovuti ya
PROFXTIGERS Largest Traders Platform
Yapo mengi ya kuwaambia ila Haya ni machache ya kuzingatia ili iwe safari ya kudumu na yenye mafanikio. Usisahau kumshirikisha na mwenzako.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad