Hiki ndicho Lema atakachokisema akikutana na Rais Magufuli

Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema amesema siku akikutana wa Rais wa Tanzania, John Magufuli atamueleza jinsi viongozi aliowateua walivyojaa hofu na kushindwa kufanya uamuzi.

Lema akizungumza na wananchi wa jimbo lake amesema hofu hiyo inawafanya viongozi kushindwa kufanya uamuzi, kwamba hofu hiyo sasa imewakumba hadi wanasiasa ambao baadhi wanalazimika kuhama vyama vyao na kutokuwa wa kweli.

Amesema Chadema kinawataka viongozi walioteuliwa na kiongozi mkuu huyo wa nchi kuondoa hofu katika utendaji wao wa kazi ili waweze kutekeleza shughuli za maendeleo wanazozisimamia.

Akizungumza katika mkutano huo, Diwani wa Ngarenano (Chadema), Isaya Doita amesema  maendeleo katika jijini Arusha yanatokana na kazi nzuri ya baraza la madiwani la Chadema.

Lema alisimamishwa kuhudhuria mikutano mitatu ya Bunge kutokana na kuunga mkono kauli ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Mussa Assad kuwa Bunge la Tanzania ni dhaifu.

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Ni kweli kwani karibia miaka yote ilikuwa kazi hufanywa kama upendavyo na hakuna mambo ya kutumbuliwa. Lakini mbona Lukuvi, Ummy, Bwana Mpango, Palamagamba na Bwana Adukadir Mruma hawana hofu? Nafikiri ukiijua kazi yako vizuri, unakuwa mbali na hofu.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad