Takriban watu 26 , akiwemo imwandishi wa habari na raia wa kigeni kadhaa wameuawa katika shambulio la katika mwambao wa kusini mwa Somalia wa Kismayo. Vikosi vya usalama katika mji wa vimemaliza makabiliano ya usiku kucha na wanamgambo walioishambulia hoteli maarufu na kuwauwa watu karibu 10.
Miili ya watu waliouawa imeondolewa kutoka kwenye hoteli hiyo huku msako ukiendelea kufuatia shambulio kubwa zaidi kuwahi kutokea mjini Kismayo kwa miaka kadhaa Kismayo kwa miaka kadhaa.
Majeruhi wa shambulio hilo wanapatiwa matibabu na baadhi wamewasili leo mjini Nairobi Kenya kwa ndege kwa ajili ya matibabu zaidi.
Shambulio ambalo lilianza kwa mlipuko wa bomu la kutegwa ndani ya gari lililokuwa kwenye lango la hoteli ya Easey lilidumu kwa muda wa saa kadhaa huku vikosi vya usalama vikikabiliana na wapiganaji waliokuwa na silaha nzito hadi asubuhi.
Image caption
Wanamgambo wa Alshaabab wanasemekana kugonga gari lililokuwa limesheheni vilipuzi
Miongoni mwa watu waliouawa ni pamoja na mwandishi wa habari maarufu mwenye uraia wa Canada na Somalia Hodan Nalayeh na mumewe.
Walioshuhudia wanasema maafisa wa ngazi ya juu wa kisiasa akiwemo mgombea wa urais katika uchaguzi ujao katika jimbo la Jubaland pia aliuawa.
Hodan atakumbukwa kwa kazi yake katika kuwapa moyo vijana na kupigania amani na ujenzi upya wa nchi ya Somalia iliyokumbwa na vita.
Alianzisha Intergration TV -kipindi kilichopeperusha matangazo yake kwa lugha ya kiingereza kupitia mtandao ambapo alitangaza vipindi juu ya hadithi na taarifa kuhusu maisha nchini Somalia na wasomali wanaoishi nchi za kigeni.
Vyombo vya habari katika eneo hilo na muungano wa waandishi wa Somali unasema kuwa Nalayeh ,43, pamoja na mumewe ni miongoni mwa wale waliouawa.
Idadi ya watu waliouawa katika shambulio la uvamizi wa alshabab yafikia watu 26
0
July 13, 2019
Tags