IGP Sirro Aridhishwa Na Ujenzi Wa Nyumba 10 Za Askari Polisi Shinyanga

Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania (IGP)  Simon Sirro ameipongeza kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa wa Shinyanga kwa Usimamizi mzuri katika ujenzi wa nyumba 10 za askari polisi ambazo zimegharimu shilingi milioni 225.

Pongezi hilo amezitoa leo baada ya kutembelea na kukagua nyumba hizo za kisasa za makazi ya askari polisi zilizojengwa katika eneo la Kambi ya polisi Kambarage Mjini Shinyanga baada ya kuridhishwa na ujenzi wake.

Amesema nyumba kwa sasa Serikali inajenga nyumba zingine za makazi ya askari polisi 400 na mpaka sasa zilizokamilika ni 114 ambazo zinajengwa katika maeneo mbalimbali hapa nchini.

Amefafanua kuwa  wanamsubiri Rais, Dkt, John Pombe Magufuli kufanya uzinduzi wa nyumba 114 zilizokamilika hapa nchini huku ujenzi wa nyumba zingine ukiwa katika hatua mbalimbali.

Ameongeza kuwa serikali ya awamu ya Tano imedhamiria kuboresha makazi ya askari poli hivyo kukamilika kwa nyumba hizo kutasaidia kupunguza  tatizo la makzi ya askari hapa nchini.

Nae mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na usalama ya mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack amemshukuru Rais Magufuli kwa kutoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa makazi ya askari polisi na  kumwomba  IGP Sirro kutafuta fedha zingine kwaajili ya ukarabati wa baadhi ya nyumba za askari ambazo hali yake siyo nzuri.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad