Iran imetoa picha ya meli iliyokamata ''ikisafirisha mafuta kimagendo" Alhamisi iliyopita
Iran inadai kuwa imewakamata majasusi 17 ambao inasema wamekuwa wakifanyia kazi shirika la ujasusi la Marekani CIA, na kuwahukumu kifo baadhi yao.
Wizara ya Intelijensia imesema kuwa washukiwa hao wamekuwa wakikusanya taarifa kuhusu mpango wa nyuklia, jeshi na sekta zingine nchini humo.
Rais wa Marekani Donald Trump, amepuuzilia mbali madai hayo akisema kuwa ni ''uwongo mtupu".
Mzee Mwinyi akerwa na January Makamba
Ronaldo hana kesi ya kujibu
Mtembo: Mti wa usuluhisho huko Mwika Tanzania
Washington na Tehran zimekuwa zikizozana kuhusu mpango wa nyuklia wa Iran na hali ya taharuki imekuwa ikiongezeka kati ya mataifa hayo mawili.
Mwaka jana Bw. Trump aliiondoa Marekani katika mkataba wa kimataifa wa nyuklia wa Iran na kuliwekea upya vikwazo vya kiuchumi taifa hilo.
Katika wiki za hivi karibuni mataifa hayo yalikaribia kukabiliana kijeshi katikaeneo la Ghuba.
Akizungumza muda mfupi baada ya tangazo lililotolewa na Iran kuhusu kukamatwa kwa maafisa hao, Trump alisema: " inakuwa vigumu kwangu kufikia mkataba na Iran."
Tunafahamu nini kuhusu 'kesi ya ujasusi'?
Iran inasema kuwa majasusi wanaoaminiwa kufanyia kazi Marekani wamekamatwa katika kipindi cha miezi 12 hasi mwezi Marchi mwaka huu.
Watu hao 17, wote ni raia wa Iran wanaofanya kazi katika "vituo maalum" vya kijeshi, mitambo ya nyuklia na sekta ya kibinafsi na wamekuwa wakifanya kazi mmoja mmoja, alisema afisa wa Iran wa ujasusi anayeshikilia cheo ja juu amewaambia wanahabari.
Je unafahamu uwezo wa Jeshi la Iran?
Hakusema ni wangapi waliohukumiwa kuuawa na ikiwa hukumu dhidi yao tayari imetekelezwa.
"Hukumu ya watu hawa imetolewa, na baadhi yao wamehukumiwa kifo kama 'wafisadi duniani' [Kosa ambalo adhabu yake chini ya sheria ya Kiislam inayotekelezwa nchini Iran]," Mkuu wa kitengo cha ujasusi amenukuliwa na shirika la habari la wanafunzi nchini Iran(ISNA).
Siku ya Jumapili, Waziri wa intelijensia wa Mahmoud Alavi alitangaza kuwa taarifa ya kina kuhusu kukamatwa kwa majasusi hao wanaohusishwa na Marekani itaoneshwa katika Televisheni ya Kitaifa ya Iran.
Hormuz: Kwa nini eneo hili linaweza kuathiri maisha yako duniani
Wizara ya Intelijensia ya Iran pia ametoa kanda ya video inayoonesha kionjo cha taarifa hiyo maalum, inayoangazia jinsi majasusi hao walivyokutana na pia kuwahojooi maafisa wa serikali akiwemo Bw. Alavi.
Baadhi ya majasusi hao walianguka katika ''mtego wa visa" uliyowekwa na CIA kwa raia wa Iran wanaotaka kusafiri nchini Marekani, Bw. Alavia aliongeza kuwa : "Wengine walifikiwa wakati walipokuwa wakiomba visa, huku wengine waliokuwa na visa kuanzia mwanzo wakishurutishwa na CIA kuomba wabadilishiwe upya hati hiyo muhimu ya usafiri ."
Iran Imewakamata na Kuwahukumu Adhabu ya Kifo Majasusi wa CIA
0
July 23, 2019
Tags