Iran yakanusha madai ya Marekani juu ya kukiuka mkataba wa nyuklia

Iran leo imakanusha madai ya Marekani kwamba nchi hiyo ilikiuka mkataba ya nyuklia siku nyingi. Iran ilitia saini mkataba huo na mataifa makubwa duniani juu ya kuzuia uundaji wa silaha za nyuklia.

Marekani imetoa madai hayo baada ya Iran kusema kuwa imekusanya urani iliyorutubishwa kidogo, kuvuka kiwango kinachoruhusiwa kwa mujibu wa mkataba.

Waziri wa mambo ya nje wa Iran Mohammad Javad Zarif amekanusha kwenye  Twitter, kauli iliyotolewa na msemaji wa Ikulu ya Marekani, kwamba Iran ilikuwa inakiuka mkataba hata kabla ya kuanza kutekelezwa.

Waziri Zarif ameeleza kwamba Iran inatumia haki yake ya kuijibu hatua iliyochukuliwa na Marekani ya kujiondoa kwenye mkataba wa nyuklia uliofikiwa kati ya Iran na mataifa makubwa.

Waziri huyo wa Mambo ya Nje amesema hatua ya Iran haiendi kinyume cha mkataba uliofikiwa.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad