Iran Yatishia Kuitandika Kwa Makombora Uingereza
0
July 07, 2019
Mjumbe wa baraza la wataalamu wa Iran, Ayetullah Muhammed Ali Musevi, amesema Iran itajibu mapigo kwa makombora kutokana na kitendo cha uongozi wa Gibratar ambayo ni sehemu ya Uingereza, kuikamata meli ya mafuta ya Iran.
Akiongea na shirika la habari la Fars Musevi ameionya Uingereza kutokana na kitendo cha meli ya mafuta ya Iran kukamatwa katika mlango bahari ya Gibrata.
Musevi alikumbushia jinsi Iran ilivyoidungua ndege isiyoendeshwa na rubani ya Marekani baada ya kukiuka na kuingia katika anga la Iran bila ruhusa, kisha akasema kwamba kamwe Iran haitakubali kuonewa na kuhusiana na suala la meli yao kushikiliwa watatoa majibu muafaka.
Musevi alisema anatangaza waziwazi Uingereza ni budi iogope kushushiwa makombora na Iran.
Baada ya Uongozi wa Gibrata ambayo ipo chini ya Uingereza kuikamata meli ya mafuta ya Iran iliyokuwa ikipeleka shehena Syria siku ya alhamisi, Iran ilielekeza vitisho vya kuipiga kwa makombora Uingereza.
Tags