IRENE Uwoya Embu Kuja Hapa Tumalize Hii Kesi...


MWANANGU Irene Uwoya. Ni mimi hapa baba yako wa kufukia. Nakuita Mama Krish kwa cheo cha mjukuu wangu ili kuonesha msisitizo.

Mama Krish, unajua sana ninavyokuheshimu na ninavyokupenda. Najua pia unaniheshimu binti yangu.

Kwa kuwa tangu jana nahaha kutafuta video yako inayosemwa wenye connection wanayo. Na kwa vile usiku mzima nimekesha nikiitafuta bila mafanikio.

Na kwa kuwa unafahamu mimi baba yako sina connection mjini, hivyo ni vigumu sana kuipata.

Sasa basi, kwa heshima na taadhima, naomba unitumie video hiyo wewe mwenyewe ili nisiendelee kuhangaika. Nimechoka mwanangu. Nitumie nipumzike, nipate na usingizi tafadhali.

Kwa wale ambao hamna connection. Ambao siku nzima jana hamkufanya kazi, mnahangaika kuitafuta video ya binti yangu Mama Krish. Labda mlikesha kama mimi. Nawaomba mrejee kazini. Chapeni kazi msubiri mpaka mwanangu Irene anitumie. Teh teh teh!

Natanguliza shukurani za dhati!

Ndimi Babu Krish
from @luqmanmaloto

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad