Jaguar Aachiwa Huru Kwa Dhamana, Kesi Kuendelea Kusikilizwa
0
July 03, 2019
Mbunge wa Jimbo la Starehe nchini Kenya, Charles Njagua, maarufu kama Jaguar, ameachiwa huru leo Jumatano Julai 3, 2019 baada ya kuzuiliwa mahabusu kwa siku tano.
Jaguar ameachiwa huru leo Julai 3 kwa dhamana ya Ksh 500,000 ambayo ni sawa na shillingi za Kitanzania milioni 11, laki mbili na elfu 7.
Akitoa uamuzi wake hakimu mkuu wa mahakama ya Milimani Francis Andayi alisema Jaguar ana majukumu ya kuwalinda Wakenya na raia wote wa kigeni na iwapo atatoa matamshi ya aina hiyo tena, atachukuliwa hatua kali zaidi za kisheria
Ikumbukwe kuwa Mbunge huyo alikamatwa kwa kutishia kuwafukuza wafanyabiashara wa nchi za kigeni wakiwemo Tanzania na uganda kutoka Kenya kwa madai kwamba wageni hao wamewapokonya Wakenya biashara zao.
Katika kliou ya video iliyozagaa, ilimuonyesha Mbunge huyo akisema Raia hao wa Kigeni waondoke ndani ya Masaa 24 la sivyo watatumia nguvu kuwaondoa ikiwemo kuwapiga hatua ambayo ilizua mtafaruku kwani wengi walionyesha kuchuizwa na kauli hiyo.
Kesi dhidi ya Mbunge huyo wa Starehe inategemewa kusikilizwa tena Julai 17 mwaka huu.
Tags