Jeshi la Sudan lasaini makubaliano ya kugawana uongozi na upinzani
0
July 17, 2019
Jeshi la Sudan limesaini makubaliano ya kugawana uongozi na upinzani.
Baraza tawala la kijeshi na viongozi wa upinzani nchini Sudan, wamesaini makubaliano ya kugawanya uongozi baada ya mazungumzo ya usiku kucha kumaliza mzozo nchini humo.
Kumefanyika sherehe zilizomalizika hivi punde katika hoteli ya Corinthia katika mji mkuu wa Khartoum.
Kuna matumaini ya kuwepo kwa Sudani mpya?
Jeshi la Sudan laitisha uchaguzi mkuu
Muungano wa Afrika AU waipiga marufuku Sudan
Makubaliano hayo yanatazamia miaka mitatu ya uongozi wa pamoja utakaofuatwa kwa uchaguzi mkuu.
Baada ya kusainiwa kwa makubaliano hayo, viongozi wa pande zote wamezungumzia kizazi kipya katika taifa ambalo limeshuhudia ghasia na maujai ya mamia ya waandamanaji tangu kutimuliwa kwa kiongozi aliyekuwepo Omar El Bashir mnamo April.
Tags