John Bocco achaguliwa kuwa Nahodha wa Taifa St


Kocha Etiene Ndayiragije amemteuwa John Bocco kuwa Nahodha wa Taifa Stars kuelekea michuano ya CHAN huku akisaidiwa na Juma Kasseja, Kelvin Yondani na Erasto Nyoni. 

Siku ya Jumapili, Tanzania itamenyana na Kenya jijini Dar es salaam kabla ya mechi ya marudiano siku ya mapema mwezi Agosti jijini Nairobi. 

Fainali ya kwanza ya CHAN iliandaliwa mwaka 2009 nchini Ivory Coast na DRC kuwa mabingwa wa kwanza. Morocco walikuwa wenyeji walikuwa wa mwisho kuandaa michuano hii mwaka 2018.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad