Julius Mtatiro Aanza Kivingine Tunduru


Mkuu wa Wilaya ya Tunduru, Julius Mtatiro, amewakaribisha wawekezaji nchi nzima kujitokeza kuwekeza wilayani Tunduru, akisema kuwa Wilaya yake imetenga kiasi kikubwa cha ardhi kwa uwekezaji.

Read More: Nafasi za Ajira 59 Zilizotangazwa Leo

Mtatiro ametoa kauli hiyo ikiwa ni siku chache tangu aapishwe kuwa Mkuu wa Wilaya hiyo, ni kuanza utekelezaji wa agizo la Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, aliloltoa hivi karibuni wakati akizindua fursa za uwekezaji mkoani Ruvuma.

"Tunduru tuna maeneo ya uwekezaji tena uwekezaji wa kutosha, tumetenga maeneo ya kutosha kwa ajili ya kuwekeza, sasa maeneo yote yameshatengwa na mwekezaji akija hapa kwetu tunampa hati ya eneo anaenda kuanza kazi.", amesema Julius Mtatiro.

Hivi karibuni akiwa mkoani Ruvuma, Waziri Mkuu Majaliwa aliwataka Wakuu wa Mikoa kutenga wiki maalum kwa ajili ya kuitumia kuitangaza Mikoa yao, juu ya fursa za uwekezaji zilizopo kwenye mikoa yao.

Julai 14, Rais wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli alitangaza kumteua Julius Mtatiro kuwa Mkuu wa Wilaya ya Tunduru akichukua nafasi ya aliyekuwa Mkuu wa Wilaya hiyo Juma Homera ambaye aliteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Katavi.

Read More: Nafasi za Ajira 59 Zilizotangazwa Leo

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad