Kaka Amuua Mdogo Wake Baada ya Kumfuma Anafanya Mapenzi Nyumbani


Mkazi wa kijiji cha Bugoshi kata ya Uyogo wilayani Kahama, Suzana Bundala (21) ameuawa kwa kupigwa na kaka yake Daudi Bundala baada ya kukutwa amelala na mpenzi wake nyumbani kwao.

Kaka yake alimkuta Suzana akiwa amelala na mpenzi wake Eddy Nkimbila kama mme na mke ndani ya nyumba yao jambo ambalo lilimuumiza

Kwa Mujibu wa Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga, Richard Abwao, tukio hilo limetokea Julai 12,2019 majira ya saa tano usiku ambapo Daudi Bundala alimuua dada yake kwa kumpiga na kitu kizito kichwani.

“Chanzo cha tukio hilo ni marehemu kukutwa akiwa amelala na mpenzi wake aitwaye Eddy Nkimbila nyumbani kwao kitendo ambacho kilimchukiza mtuhumiwa”,ameeleza Kamanda Abwao.

Amesema mtuhumiwa wa mauaji hayo alikimbia baada ya tukio hilo na juhudi za kumtafuta na kumkamata zinaendelea.

Kamanda alisema mwili wa marehemu umekabidhiwa kwa ndugu zake kwa taratibu za mazishi.

“Natoa wito kwa wananchi wa Mkoa wa Shinyanga kuacha kujichukulia sheria mkononi na kufikia kufanya matukio ya kikatili kama hili, kwani sheria zitachukua mkondo wake,”alisema Kamanda.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad