Kampuni ya Facebook yakiri kukabiliwa na matizo ya kiufundi

Baadhi ya watumiaji wa Facebook, Instagram na WhatsApp walishindwa kuweka picha, video na mafaili jana jioni.

Facebook, inayomiliki App zote tatu, imesema inafahamu kuhusu tatizo hilo na ilikuwa ''ikifanyia kazi ili kurudisha kila kitu sawa haraka iwezekanavyo''.

Mitandao ya kijamii, ina mabilioni ya watumiaji wake ulimwenguni.

Washindani wake Twitter pia walikuwa na tatizo kwa watumiaji wake kushindwa kutuma ujumbe wa moja kwa moja au kupokea taarifa kuhusu ujumbe ulioingia.

Kampuni iliomba radhi kwa dosari hiyo kupitia ukurasa wake wa Twitter wakisema kuwa wanashughulikia tatizo hilo.

Watumiaji bado waliweza kuweka ujumbe kwenye twitter na ujumbe wa hashtag #instagramdown ukaanza kushika kasi mtandaoni wengi wakitumia kueleza matatizo ya mshindani wake.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad