Kampuni ya Kimataifa ya inayojishughulisha na Miundombinu ya Ujenzi wa Viwanja vya Ndege, Gati pamoja na Nyumba ya OZUAYDIN kutoka Nchini Uturuki imeonyesha imesema ipo tayari kushirikiana na Serikali ya Mapinduzi ya Zanziar katika uimarishaji na ujenzi wa Bandari mpya Visiwani humo.
Hayo yalielezwa na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni hiyo, Ezpa Vildiz Sasmaz wakati wa Mazungumzo na na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Ofisin kwake Vuga Mjini Zanzibar, alipokwenda akifuatana na Ujumbe wa Viongozi wa Nne wa Kampuni.
Mkurugenzi huyo alisema kuwa Kampuni yake ipo tayari kushirikiana na Serikali ya mapinduzi ya Zanzibar katika kuimarisha na Ujenzi wa Bandari Mpya ndani ya visiwa vya Zanzibar.
Alisema Kampuni ya OZUAYDIN iliyoasisiwa mnamo Mwaka 1982 imefanya utafiti na kuridhika na harakati za kibiashara zinazofanyika Visiwani Zanzibar ambazo Kampuni yake imeona ipo haja ya kutumia taaluma iliyonayo katika kuongeza nguvu za uwajibikaji katika eneo hilo la Biashara.
Alisema ujenzi wa Bandari mpya ya Kisasa Zanzibar ambayo Kampuni yake ina kila sifa na uwezo wa kujenga miundombinu inaweza kuongeza kasi ya Biashara kwa vile mfumo unaotumiwa katika ujenzi huo unazingatia wakati wa sasa wa sayansi na Teknolojia.
Ezpa Vildiz Sasmaz alimuhakikishia Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kwamba Mradi huo endapo utafanikiwa katika azma ya Kampuni hiyo Bandari ya Zanzibar inaweza kuwa tegemeo kubwa la Uchumi wake kutokana na kuongezeka kwa harakati za Kibiashara kupitia Mlango huo wa Gati Kiuchumi.
Akitoa shukrani zake Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema uwepo wa Bandari Mpya Zanzibar kutokana na mabadiliko ya Biashara yaliyopo hivi sasa ni muhimu katika kuchangia mapato ya Taifa.
Balozi Seif alisema Bandari ya Malindi iliyopo hivi sasa inayotegemewa kupokea mizigo mikubwa kutoka Mataifa ya nje hasa Makontena ya bidhaa mbali mbali ni ni ndogo kutokana na msongamano mkubwa wa mizigo inayoteremshwa na meli tofauti.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi aliushauri Uongozi wa Kampuni hiyo ya OZUAYDIN kuandika maombi yaliyokamilika ya Mradi huo wa Ujenzi wa Bandari ili Serikali ipate wasaa wa kuupitia na kuona namna itakavyoweza kushirikiana na Kampuni hiyo katika utekekelezaji wake.
Kampuni ya Kimataifa ya inayojishughulisha na Miundombinu ya Ujenzi wa Viwanja vya Ndege, Gati pamoja na Nyumba ya OZUAYDIN imeonyesha nia ya kutakja kuijenga upya Banadari ya Malindi kutokana na harakti zake zinazoonekana kuleta msongamano mkubwa wa bidhaa na mizigo inayoingia na iule inayotoka.