Kauli ya Dk. Bashiru Juu ya Wanaotekwa na Watu Wasiojulikana na Kupotea


Kufuatia tuhuma mbalimbali za matukio ya utekezaji zinazotolewa na wanasiasa mbalimbali, Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) nchini Tanzania, Dk. Bashiru Ally ameweka mkazo kwamba hakuna ukweli wowote na si sahihi kuihusisha serikali na na matukio hayo.

Akizungumza wakati akiwa ziarani katika Kata ya Naisinyai, wilayani Simanyiro mkoani Manyara jana, Dk. Bashiru amesema kwamba baadhi vyama vya siasa vinatoa taarifa potofu juu ya vitendo vya utekeji na watu kupotea huku wakiihuisha serikali.

“Ulinzi na usalama ni wajibu wa Serikali, baadhi ya watu kuihusisha (Serikali) na watu wasiojulikana wanaoteka watu hapo watakuwa wanaoichonganisha na watu wake,” amesema Bashiru huku akibainisha kuwa mwenye jukumu la kutoa taarifa katika Mkoa ni Mkuu wa Mkoa na kamanda wa polisi wa Mkoa.

“Hao wawili ndio wanapaswa kutoa taarifa ya hali ya ulinzi na usalama ya Mkoa na si viongozi wengine wanaochafua hali ya hewa kwenye mitandao ya kijamii,” amesema Bashiru.

Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Alexander Mnyeti wakati akisoma taarifa ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo ya mkoa huo, amesema serikali imepiga hatua kwenye miradi mbalimbali ikiwemo ya elimu, afya, miundombinu ya barabara, umeme na maji.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad