Keisha Atumbuliwa Nafasi ya Ujumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Sababu za Kung’olewa zatajw
0
July 02, 2019
Chama tawala cha Mapinduzi (CCM) kimefanya mabadiliko madogo ya Kamati Kuu ya chama hicho kwa kumuengua, Khadija Shabani almaarufu kwa jina la Keisha baada ya kuitumikia kamati hiyo kwa takribani mwaka mmoja.
Keysha aliteuliwa kwenye kamati hiyo ambaye pia ni msanii wa muziki wa kizazi kipya, Aliteuliwa mwezi Mei 28 mwaka jana, Uteuzi ulioambatana na teuzi za Waziri Mkuu Mstaafu, Mizengo Pinda na mtoto wa hayati Mwl. Julius Nyerere.
Msanii huyo wa muziki, Wengi waliamini kuwa angekuwa kiungo muhimu katika uhamasishaji wa sera za chama kwa wasanii wenzake nchini Tanzania.
Uamuzi huo wa kung’olewa kwa Keisha, Ulitangazwa Ijumaa iliyopita ya Juni 28 katika kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) kilichofanyika Jijini Dar es Salaam na kuongozwa na mwenyekiti wake, Rais Magufuli.
Nafasi ya Keisha kwa sasa imechukuliwa na Munde Tambwe ambaye ni mbunge wa Viti Maalumu kutoka Mkoa wa Tabora.
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa chama hicho, Humphrey Polepole akizungumzia maamuzi hayo amesema kuwa “Halmashauri Kuu ya Taifa ina mamlaka ya kupanga na kupangua ili kuongeza tija na kutumia ujuzi na umahiri wa wajumbe katika kuongeza tija na ushindi wa CCM.”.
Kuhusu sababu za kuenguliwa kwa Keysha, Imeelezwa kuwa amekuwa akituhumiwa kuvujisha siri za ndani za kamati hiyo nyeti ya Chama kikongwe barani Afrika.
Tags