Kenyatta Amaliza Ziara Yake Chato

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta, ammaliza ziara yake ya siku mbili nchini Tanzania na kurejea nchini mwake. Katika ziara yake hiyo Kenyatta, amemjulia hali mama mzazi wa Rais Dkt. John Magufuli ambaye anaendelea na matibabu nyumbani kwake Chato, Geita.



Kenyatta ameagana na mwenyeji wake, Rais Magufuli katika Uwanja wa Ndege wa Chato. Katika ziara hiyo, marais hao wamesisitiza kudumisha amani na uhusiano mzuri katika nchi za Jumuiya Afrika Mashariki na kushirikiana katika mambo mbalimbali ikiwemo biashara.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad