Kijana Afariki Baada ya Kutumbukia Kisimani

Ali Ibrahimu Haji (30), Mkazi wa Jambiani Kibigija amefariki dunia baada ya kutumbukia kisimani katika Bar ya Maisha Pub Mkoa wa Kusini Unguja

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kusini Unguja, Suleiman Hassan Suleiman amesema kuwa tukio hilo lilitokea jana Usiku

Daktari katika Hospitali ya Makunduchi Cottage amesema kuwa wamepokea maiti hiyo na kuifanyia uchunguzi na kuikuta ina majeraha madogo huku chanzo chake ikisadikiwa kushindwa kupumua na kuhimili maji ya kisima hicho

Naye Diwani wa Jambiani amesema kuwa marehemu inasadikiwa alikuwa amelewa na kabla ya kufariki aliondoka katika meza na kuelekea msalani na ndipo alipoingia katika kisima
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad