Kim Kardashian Aamua Kubadili Jina la Nguo za Ndani

Kim Kardashian West anajipanga kubadilisha jina la nguo zake za ndani kufuatia shutuma kali za kudunisha mila.

Raia wa Japani wanaotumia mitandao ya kijamii walishutumu vikali jina la kibiashara la nguo hizo, Kimono.

Kimono ni jina la vazi la taifa na kitamaduni nchini Japani.

Awali Bi Kardashian, alijitetea na kusema hatobadili jina hilo, akisema halikuwa lengo lake kukashifu vazi au utamaduni wa jamii fulani.

Lakini leo Jumanne, amesema kuwa atatangaza jina lengine la nguo hizo hivi karibuni.

Ruka ujumbe wa Instagram wa kimkardashianMwisho wa ujumbe wa Instagram wa kimkardashian
Nyota huyo wa Televisheni, mwanamitindo na mbunifu wa mavazi ameandika kupitia ukurasa wake wa Instagram kuwa: "Kila siku nasikiliza watu, najifunza na kukua… Nilipotangaza jina la nguo zangu, nilifanya hivyo nikiwa na nia njema moyoni."

Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image caption
Kimono ni vazi rasmi nchini Japani toka Karne ya 16
Ameongeza: "Baada ya kulifikiria kwa kina, nitazizindua tena kwa jina jipya."

Kimono, ambalo ni vazi refu kama gauni linalofungwa na mshipi, limekuwa vazi rasmi la taifa la Japani toka Karne ya 16, na linaendelea kuwa vazi rasmi la taifa hilo.

Yuka Ohishi, mwanamke raia wa Japani wiki iliyopita aliiambia BBC kuwa: "Tunavaa kimono kusherehekea afya, kukua kwa watoto, pamvu, mahafali, ndoa na misiba. Ni vazi la sherehe toka jadi na jadi.

"Hizo nguo zake za ndani hazifanani kabisa na kimono - amechagua jina hilo kwasababu ndani yake kuna Kim - hakuheshimu kabisa vazi hilo lina maana gani kwenye utamaduni wetu."

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad