Kinana Atuhumiwa Kujihusisha na Ujangili wa Meno ya Tembo


Katibu Mkuu Mstaafu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana ametuhumiwa katika kashfa nzito ikiwamo ya kujihusisha na biashara ya meno ya tembo.

Tuhuma hizo zilitolewa na Mwanaharakati Huru, Cyprian Musiba wakati akizungumza na waandishi wa habari alieleza kuwa mbali na tuhuma hizo Kinana aliuza ardhi pamoja na kuwatukana mawazi kwa kuwaita ni mizigo wakati alipozunguka nchi nzima na kuzua taharuki katika serikali ya awamu ya nne.



‘Nani alimtuma akaite mawaziri kuwa ni mizigo alikuwa na kashfa ya kuwa miongoni mwa Watanzania waliojihusisha na ujangili, madawa ya kulevye hizo kashfa hazijathibitika lakini alidaiwa kuua tembo wetu,” alisema

Aliongezea kuwa:”Leo hii huyo Zitto Kable anajifanya kumtetea Kinana wakati alikuwa anaongoza mashambuliza ya Kinana kuua tembo wetu, faru walitaka kuondoka wote, twiga walikuwa wanapandishwa kwenye ndege alafu leo Zitto unatetea mambo hayo kweli yaani Zitto angekuwa karibu ningempiga vibao ni mjinga kabisa,”alisema

Aidha, Musiba alisema anachokieleza hatumwi na CCM, wala serikali wala Ikulu yeye ni mwanaharakati huru anaruhusiwa kuongea kwa mujibu wa katiba bila kuvunja sheria.

“Asiyejua kama Kinana alikuwa na meli inayosafirisha meno ya tembo ni nani? Kinana alihusika na uuzaji wa mtambo wa kuchapa magazeti ya CCM hizo ndio hoja ambazo wanatakiwa waje kujibu sio kunishambulia mimi ule mtambo uliuzwaje? Waliuzia Jamana Printers na upo Mwanza waje kujibu hoja,” alisema

Aidha, alisema Kinana alihusika katika mikataba mibovu na kuiingiza chama katika madeni makubwa.

“Vumilieni hii dewa iwaingie Kinana ajibu kuhusu mashine za kufulia zilizoletwa kama msaada na wahisani kwenda katika hospitali ya Mount Meru lakini msaada huo ukayeyuka na kumpatia mdogo wake ambaye alifungua Dry  Clean mkoani Arusha,” alisema Musiba.

Aliongezea kuwa:”Kinana hawezi kurudi aliyoyafanya ni mazito kwa sasa yupo nchini Canada na yule ni raia wa nchi mbili Tanzania na Canada,” alisema Musiba.

Kinana alipotafutwa kuzungumzia tuhuma hizo kwa njia ya simu  hakupatikana.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad