Kinana na Makamba Wapongezwa Kwa Ujasiri wao wa Kumkaanga Musiba



Hakuna mwana-CCM ambaye alikuwa hachukizwi na tabia ya  Cyprian Musiba ya kuwachafua na kuwadhalilisha viongozi wetu wa CCM wa sasa na wastaafu.

Kwa hakika vitendo vya Musiba vilikuwa vinachonganisha na kuleta mpasuko na mgawanyiko kwenye Chama chetu. Musiba alifikia hadi kusema kwamba Makamu wa Rais wa Zanzibar anafanya njama za kumhujumu Rais Magufuli.

Lakini pamoja na yote haya, hakuna mtu aliyefungua mdomo na kumkanya.

Sasa wazee wafia CCM ambao wamezeeka wakiitumikia CCM, wameamua kusema yale ambayo sote tumekuwa tunayafikiria. Wametukumbusha CCM ya Nyerere, kwamba linapotokea jambo la kuhatarisha umoja na amani ya nchi linakemewa haraka, tena kwa sauti kubwa, tena hadharani.

CCM sio ya mtu mmoja au kikundi cha watu. CCM ni Chama ambacho wote tumekikuta. Tumekikuta kwasababu kilikuwa na mila, desturi na utamaduni uliokidumisha. Moja ya mila hizo ni kwamba hatukodishi mamluki na vichaa kuisemea Serikali na kumtetea Mwenyekiti wetu. Kazi hiyo tunaifanya wenyewe. Mila nyingine ni kwamba tunaheshimu viongozi wetu wastaafu waliokitumikia Chama, na ndio maana tunawaalika na kuwapa nafasi kwenye mikutano yetu mikuu.

Tukikaribisha mila, desturi na utamaduni mpya wa kufanya siasa kwenye Chama, ambapo vichaa wa kukodishwa ambao hata hawakutafuta kura za Magufuli ndio wanaruhisiwa kujionyesha ukereketwa na kutukana viongozi, basi sote kitatufia mikononi mwetu.

Tunawashukuru Wazee wetu Makamba na Kinana kwa kuonyesha njia.

Ni sisi,
Mtandao wa Waenezi wa CCM wa Wilaya – Tanzania Bara
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad