Kiongozi mkubwa wa upinzani nchini Urusi ambaye pia ni mkosoaji wa Serikali ya Rais, Vladimir Putin, Alexei Navalny jana jumatatu amehukumiwa kwenda jela kwa siku 10 mjini Moscow. Baada ya kukutwa na hatia ya kushiriki maandamano yasiyo halali mwezi uliopita, yaliyokuwa na lengo la kushinikiza muandishi wa habari za kiuchunguzi, Ivan Golunov aachiwe huru.
Maandamano hayo yaliyofanyika Juni 12, mwaka huu. Yalipelekea watu zaidi ya 400 kukamatwa na mpaka leo kuna wengine bado wanashikiliwa na vyombo vya usalama nchini humo.
Ivan Golunov alikamatwa kwa tuhuma za kujihusisha na madawa ya kulevya, Tuhuma ambazo zilifutwa baadae baada ya kukosekana kwa ushahidi.