Derby imemruhusu kocha Frank Lampard asihudhurie mazoezi ya kabla ya msimu kuanza, wakati klabu hiyo ikimtarajia kupata nafasi ya kukifundisha kikosi cha Chelsea.
Lampard hatakuwepo kwenye mazoezi siku ya Jumatatu au Jumanne wakati mazungumzo yakiendea na klabu ya Chelsea, ambayo aliichezea kwa miaka 13.
Derby alifanya maamuzi hivyo uhamisho huo ''utakamilika haraka iwezekenavyo''.
Kama Lampard ataondoka, Derby inategemea kutangaza atakayechukua nafasi yake mwishoni mwa juma.
Kocha msaidizi wa Rams, Jody Morris pia hatakuwepo mazoezini.
Kuna hisia kuwa Morris atahamia Chelsea pamoja na Lampard, Kiungo wa zamani wa England atamrithi Maurizio Sarri, ambaye ameondoka Stamford Bridge na kujiunga na Juventus mwezi uliopita.
Wachezaji wa Derby watafanya vipimo vya afya siku chache zijazo, hivyo klabu inaona kuwa itakuwa inaendelea na majukumu yake bila kuwa na Kiongozi.
Kikosi kinatarajia kusafiri kwenda Florida kwa ajili ya kambi ya mazoezi siku ya Alhamisi.
Taarifa ya Derby iliyotolewa siku ya Jumatatu imesema: ''Siku chache za mwanzo za kabla ya msimu kuanza wataanza na mazoezi ya viungo na wataendelea kwa kuzingatia muongozo wa wataalamu wa viungo, kitabibu na sayansi ya michezo.
Nahodha wa zamani wa Chelsea, John Terry kwa sasa kocha msaidizi wa Aston Villa, amesema ''hakuna mwenye uwezo'' wa kuiongoza Chelsea isipokuwa mchezaji mwenzake wa zamani.
Lampard ameonekana akiichezea Blues mara 648, na kushinda makombe 11 na kikosi hicho, baada ya kujiunga akitokea West Ham kwa kitita cha pauni milioni 11 mwaka 2001.
Lampard made 648 appearances for the Blues, winning 11 major trophies with them, after joining from boyhood club West Ham for a fee of £11m in 2001.