Kupatwa kwa mwezi 16 - 17 Julai


Mamlaka ya hali ya hewa nchini TMA, imesema usiku wa Julai 16 - 17, kutatokea hali ya kupatwa kwa mwezi, ambapo tukio hilo hujirudia mara chache sana katika maeneo husika.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na mamlaka hiyo, imeeleza kuwa tukio hilo ni la kupatwa kwa mwezi sehemu (Penumbra), ambalo litaonekana katika nusu ya Dunia, hususani maeneo ambayo tarehe hiyo itakuwa usiku, ikiwemo Ulaya, Asia, Australia na Afrika.

Kwa mujibu wa TMA, hapa nchini  hali hiyo imeonekana kuanzia jana, Julai 16 majira ya saa 3 hadi saa 9 usiku wa kuamkia Julai 17.

Aidha imeelezwa kuwa tukio hilo halina athari yoyote, ila upo uwezekano wa kuongezeka kwa kina cha maji katika bahari na kwamba hali hiyo inaelezwa kusababishwa na mvutano  kati ya mwezi na maji katika bahari.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad