Kupitia Matonya zifahamu sifa za Wanaume wa Tanga


Msanii wa muziki wa BongoFleva Seif Shabani maarufu kama Matonya, amefunguka ishu za yeye kuwa mlevi na sifa za wanaume wa mkoa wa Tanga.

 

Matonya amefunguka hayo kupitia EATV & EA Radio Digital, baada ya kuulizwa kuhusu tuhuma za yeye kuwa mlevi.


  • "Kweli mimi nakunywa lakini sijawahi kufanya vitu tofauti, nakunywa ninapo tamani na nakula pesa yangu, lakini sasa hivi nakaribia mwaka na miezi kadhaa sijagusa pombe kwenye kinywa changu, mimi ni mnywaji na sio mlevi ila nafikiri pombe ni ibilisi tu maana nakunywa bia kali na pombe kali".


Aidha msanii huyo ameeleza sifa za Wanaume wa mkoani Tanga ambako anatokea yeye na kusema, Watu kutoka Tanga ni watu makini, na Wanaume wa mkoa huo wana sifa ya ubaharia wa upandaji meli.


  • ''Dunia nzima mabaharia wanatokea mkoani Tanga, kwa sababu wao wanacheza sana na bahari''. amesema Matonya.


Zaidi mtazame kwenye Video hapa
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad