Lema awataka Viongozi wastaafu kukemea tuhuma za utekaji


Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema amewataka viongozi wastaafu kukemea vitendo vya utekaji vinavyodaiwa kuendelea nchini.

Lema amesema kuwa anaamini kuwa  siku Ridhiwan akitekwa Mh. Kikwete ataongea au Abdullah akitekwa Rais Mwinyi ataongea na kuthibitisha kuwa uzee ni hekima na utu.

"Viongozi wastaafu kemeeni utekaji unaondelea Nchini.Naamini siku Rizwan akitekwa,Mh Kikwete utaongea au Abdulah akitekwa bila shaka Rais Mwinyi atathibitisha kuwa Uzee ni hekima na utu.Vunjeni ukimya,hawa wauni hawana aibu,wanaweza kumteka hata Mama Maria Nyerere. Amka paza sauti," Lema amesema kupitia ukurasa wake wa Twitter.

Hivi karibuni kumekuwa na tuhuma za kudaiwa kutekwa kwa Msaidizi wa Benard Membe Ndg Allan Kiluvya na Raphael Ongangi aliyedaiwa kudekwa na akapatikana akiwa Mombasasa Kenya.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad