Msanii wa muziki wa Bongo Fleva, mwanadada Lulu Diva amezungumzia juu ya suala la pete ya uchumba inayosemekana amevishwa na msanii na Mbunge wa Jimbo la Starehe nchini Kenya, Charles Njagua Kanyi, maarufu 'Jaguar'.
Akipiga stori na eNewz ya EATV, Lulu Diva amesema kuwa watu wasubiri kuona kama kweli pete hiyo itapelekea ndoa ama la huku akionekana kuzunguka katika kuthibitisha asilimia 100 kama pete hiyo amevishwa na msanii huyo maarufu wa Kenya.
"Pete ni hii hapa, kama hii pete ni hatua ya kwanza basi kuna ndoa na vitu vingine vingi, kama ipo ipo tu mtaiona", amesema Lulu Diva.
"Siwezi kusema mimi sifai kupelekwa kwa wakwe hapana, ninaweza kupelekwa tena kwa wale wanaoijua dini kabisa lakini mimi miaka yangu bado haijafika ya kufanya hivyo, mimi bado mdogo", ameongeza.
Aidha Lulu Diva amewaasa watu kuacha kumuhusiaha Jaguar na vitu hivyo kwakuwa kuna mambo mengi yanaendelea nchini kwao kuhusu siasa, huku akiahidi kuwa vitu vikubwa vinakuja kwa yeye na Jaguar.