Luteni 'Feki' adakwa na Polisi kwa utapeli


Jeshi la Polisi Mkoa wa Singida linamshikilia Mtu mmoja anayejulikana kwa jina la Amiel Stephano, (29) Msukuma mkazi wa Jijini Arusha katika eneo la Mbauda kwa kosa la kujifanya Afisa wa Jeshi la Wananchi mwenye cheo cha Luteni.

Akiiongea na waandishi wa habari hii leo ofisini kwake  Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida ACP Sweetbert M. Njewike ameeleza kuwa Mtuhumiwa huyo alikamatwa siku ya tarehe 17.07.2019 majira ya saa  6:00  mchana huko katika viwanja vya ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Singida  iliyopo maeneo ya Bomani katika Manispaa ya Singida.

Kamanda Njewike ameeleza kuwa jeshi la Polisi limefanya uchunguzi wa awali na kubaini kuwa Mtuhumiwa alifika maeneo hayo kwa ajili ya kuomba nafasi ya ndugu yake ili achaguliwe kujiunga na Jeshi la kujenga Taifa wakati zoezi la usaili likiendelea huku akijitambulisha  mbele ya maafisa wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT)  kuwa yeye ni Afisa wa Jeshi la Wananchi na kuonesha kitambulisho chake chenye No. D 0595  Chenye jina la P.15705 A. S. Marco jambo ambalo lilipelekea Maafisa hao kutilia  mashaka.

Aidha ACP Njewike amesema kuwa Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na Maafisa wa Jeshi la Wananchi walifanya  upekuzi katika Gari lake lenye No.T.289 AUF aina ya TOYOTA COROLA mali ya mtuhumiwa  na kukutwa na Picha za posport size 3 za mtuhumiwa akiwa katika sare za Jeshi la Wananchi zenye cheo cha Luteni,  Mihuri minne ya Shule mbalimbali, Fedha za kitanzaniza 170,000/=, Cheti cha kuhitimu elimu ya Secondari kidato cha nne na Cheti cha Kuzaliwa cha  mtu aitwaye Aloyce  Zawadiel Solomon.

Ameendelea kutaja vitu vingine kuwa ni Vivuli vya vyeti vya elimu ya sekondari, matokeo ya chuo, Cheti cha Diploma na Cheti cha Kuzaliwa vyote vikionesha kuwa ni vya mtu aitwaye Frank Brian. Barua ya uthibitisho juu ya kusoma elimu ya Sekondari, Cheti cha kuzaliwa  na Cheti cha Matokeo ya Mtihani vyote vikionesha ni  vya Janeth Adam Mtema. Vivuli vya cheti cha kuzaliwa , cheti cha udereva na cheti cheti cha elimu ya sekondari vyote mali ya Nelson John Ntandu. Pia cheti cha kuhitimu elimu ya msingi na cheti cha kuzaliwa vya Bernad Vitalis Wilbroad.

Hata hivyo Kamanda amesema upekuzi ulifanyika kwenye chumba alichokuwa amefikia Mtuhumiwa katika Nyumba ya kulala wageni ya Rock Side view iliyopo Mtaa wa Mjengo Manispaa ya Singida  na kukutwa na fedha Tsh. 500,000/=,  Kivuli cha cha cheti cha kuzaliwa cha Ramadhan Athuman pamoja na hati ya uthibitisho ya kuhitimu elimu ya msingi, picha za passport size 12 huku baadhi ya passport zikiwa na majina ya Aloyce Solomon na Janeth Adamu Mtema, Shati mojo likiwa na karatasi yenye jina la Martini Muro.
Aidha, jeshi la Polisi linanaendelea na upelelezi zaidi na baada ya upelelezi  kukamilika mtuhumiwa atafikishwa Mahakamani

Kamana amewataka wananchi wote wa Mkoa wa Singida kujiepusha na matapeli wanaofika katika maeneo yao huku wakijitambulisha kuwa ni maafisa wa ngazi za juu za serikali hususani vyombo vya ulinzi na usalama kwa lengo la  kuwashawishi kupatiwa kazi serikalini. Wananchi wanapohitaji kazi serikalini wafuate taratibu za kuomba kazi kulingana na matangazo ya kazi husika.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad