Magufuli Afurahishwa na Mauno ya Askari Wanawake, Azani Wamekodishwa



Rais John Magufuli afurahishwa na askari wanawake wa jeshi la polisi jinsi walivyokuwa wanakata viuno katika uzinduzi wa nyumba za makazi ya askari wa jeshi la polisi magogo mkoani Geita huku akisema alizani wamekodishwa kucheza.

Rais Magufuli alisema kweli jeshi lipo vizuri viuno vinazunguka nikajua wamekodisha lakini Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Simon Sirro ameniambia ni askari hao.



“Vijana wako wa polisi huwa nawashabikiaga sana huenda hawajui wanapiga nyimbo nzuri hata TBC wanazipiga lakini nashangaa hata viuno wanajua kukatika vizuri sana nilifikiri wamekodisha ndio maana IGP nikamuuliza na huyo ni askari maana kiuono kinazunguka vizuri akaniambia hayo ni mazoezi ya jeshi la polisi,”

Aliongezea kuwa:”Hongereni sana kwamba mazoezi yote mnayajua maana yake jeshi la polisi mmeiva kisawasawa yaani mmeiva katika mambo yote ya mazoezi hiki ndicho kimenifurahisha sana na huenda ndio maana mbunge Msukuma anahitaji askari wa kike waende huko sasa IGP usimnyime mchagulie hawa wanaofanya mazoezi kama haya ya kuzunguka uwapeleke huko ila tumpe masharti akatengeneze nyumba za maskari huko yeye ni mfanyabiashara na ni mbunge lakini pia anapata fedha za maendeleo ya jimbo zinazotengwa na serikali,”

Rais Magufuli alimuomba mbunge Msukuma kujenga nyumba za askari na zitakapokamilika IGP nakuagiza umpatie hao askari wa kike aliowaomba na ole wake aache kuwatunza.

“Lakini hata Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi nimeona na haya mambo anayaweza kweli jeshi la polisi mnaweza sana,”alisema Rais Magufuli huku akishangiliwa.

Aidha, Rais Magufuli amewaomba wananchi kushirikiana na jeshi la polisi na vyombo vya usalama ili kuendelea kulinda na kudumuisha amani ya nchi.

Amewasihi wana siasa kujiepusha  kutoa maneno yanayoizalilisha vyombo vya usalama kwa lengo la kujitafutia sifa na umaarufu mbele ya wananchi.

Alisema nyumba zilizojengwa amewataka  askari hao wanatakiwa kuzitunza ili zidumu.

Aidha, amelitaka Jeshi la polisi kuongeza kasi ya ujenzi wa nyumba 286 zilizobaki kwani fedha tayari zimeshatengwa iweje zingine zikamilike alafu maeneo mengine yasikamilike kwani ucheleweshaji unasababisha gharama kupanda.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad