Mahakama nchini Nigeria imeamuru kutaifishwa kwa vito vya dhahabu pamoja na simu aina ya iPhone iliyovalishwa kasha la dhahabu vinavyomilikiwa na aliyekua waziri wa zamani wa nishati nchini humo Diezani Alison-Madueke.
Bangili, cheni, hereni pamoja na saa viliamriwa kutaifishwa baada ya hukumu kutolewa dhidi ya waziri huyo ambaye kwa sasa hajulikani alipo.
Vito na simu vyenye thamani ya fedha za Kitanzania Milioni 91, vita taifishwa ndani ya siku 14 baada ya kiongozi huyo kukumbwa na kesi ya ufisadi.