Mahakama Yatoa Hati Kukamatwa Watu Watano Kwa Kumteka MO Dewji


Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imetoa hati ya kuwakamata raia wanne wa Msumbiji na mmoja wa Afrika Kusini wafikishwe kizimbani kuunganishwa katika mashtaka ya kumteka Mohammed Dewji.

Raia hao ni wa Msumbuji Mousa Twaleb, Henrique Simbine, Daniel Manchice, Issa Tomo, Zacarious Junior na raia wa Afrika Kusini Phila Tshabalala.

Washtakiwa hao wanatakiwa kuunganishwa katika shtaka la pili na shtaka la tatu ambapo shtaka la kwanza linamkabili Twaleb ambaye anadaiwa kujihusisha na genge la uhalifu, kati ya Mei mosi mwaka 2018 na Oktoba mwaka huo akiwa nchini Tanzania na Johannesburg Afrika Kusini.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad