Mambo 10 Usiyoyajua Kuhusu Wanaume Wenye Michepuko


Wanawake wengi walio kwenye ndoa wanahangaika na waume zao kwakuwa na uhusiano wa kimapenzi na michepuko. Yafuatayo ni mambo kumi ambayo yawezekana ulikuwa huyajui kuhusu wanaume wenye michepuko:

1: Wanaume wengi wanakuwa bado wanawapenda sana wake zao wakati huo wakiwa wanachepuka. Wengi huwa wanafanya hivi ili kuona mwanamke mwengine anaweza kumridhisha kwa kiasi gani, au wanaamua kuchepuka kutokana na migogoro iliyopo ndani ya uhusiano au ndoa yao.

2: Mara nyingi, wanaume wanachepuka na wanawake wanaojuana nao. Ni rahisi sana kwa mwanaume kuchepuka na mwanamke anayejuana naye kwakuwa kwa yule asiyejuana naye vizuri, inamaanisha mchakato wa kutongoza inabidi uchukue nafasi yake, wakati mwanaume anahitaji kumaliza shida zake za kufanya mapenzi kwa muda huo. Kuanza kuzungushana na mwanamke mpya ni sawa na kuishi matatizo ya uhusiano wake kwa mara nyingine zaidi, lakini kwa mwanamke anayejuana naye, hasa anayejua mgogoro wao wa uhusiano, ni rahisi kutimiza haja za mwanaume huyu kwa kumfariji.

3: Wanaume huchepuka kuokoa ndoa zao. Wanaume wanawapenda wake zao lakini wengi hawajui jinsi ya kutatua matatizo ya ndoa yao, kwahiyo wanajikuta wakienda nje ya ndoa kuziba mapengo yaliyomo kwenye ndoa yao. Wanaume wanataka kupata kila kitu na wengi wana mawazo kwamba mchepuko utamfanya asahau matatizo kwenye ndoa yake. Baada ya hapo wanaume wanarudi kwa wake zao na kuishi maisha ya furaha—wao na wake zao—bila kutafuta suluhu ya matatizo ya ndoa yao.

4: Wanaume huwa wanajilaumu baada ya kuchepuka. Wanaume wengi wakipata matatizo kwenye ndoa zao hukimbilia kwa michepuko kujaribu kupoza machungu yoyote waliyoyapata na mara baada ya kumaliza starehe alizofata hujikuta akijilaumu kwa kumsaliti mkewe na kutofanya jitihada ya kutafuta suluhu ya matatizo ya ndoa yao.

5: Wanaume wengi wenye michepuko hujificha wanapoanzisha uhusiano wa nje. Kujificha huku kunatokana na wao kujua wazi kwamba wanachokifanya si sahihi hivyo hawataki kuwasababishia machungu wake zao wakiwa na ufahamu kwamba matatizo yaliyopo kwenye ndoa yao hayana haja ya kuchochewa zaidi kwa kufanya uhusiano na mchepuko kuwa wazi kwa watu wengi, jambo litakalomuumiza zaidi mkewe.

6: Wanawake nao wanachepuka kwa spidi ileile ya wanaume na uhusiano huu ambapo mwanamke huwa anachepuka huwa ni hatari zaidi ya yale ambayo mwanaume ndiye anayechepuka. Utafiti uliofanywa na Chuo Kikuu cha Indiana nchini Marekani unaonesha kuwa wanaume na wanawake wanachepuka kwa uwiano sawa, lakini sababu zao za kuchepuka ni tofauti. Wameeleza kwamba wanawake wanapochepuka huwa ni kutokana na sababu za kujiridhisha kihisia. “Kuchepuka kwa mtandao—bila uhusiano wa kimwili—ni uchepukaji wenye madhara makubwa zaidi,” utafiti huo umebaini. Kutengeneza uhusiano wa kihisia (kinachofanywa na wanawake) na mtu mwingine inamaanisha umekubali kuachana na ndoa yako. Lakini kama ni muingiliano wa kimwili tu (unaofanywa na wanaume) huwa na hauumizi sana kwakuwa huchukuliwa ni kitendo kinachomuumiza mwenzio tu, na si kwamba amemponda mtu kihisia.

7: Mara nyingi mke huwa anajua kwamba mumewe ana mchepuko. Ingawa mwanaume huwa anadhani anajificha au anaficha uhusiano wake na mchepuko ili kuepuka kumuumiza mkewe, imebainika kuwa mara nyingi sana mke huwa anajua kuhusu mchepuko huo ila anabaki kuangalia nyendo za mumewe kuona kama zitasaidia kupoza mtafaruku uliopo kwenye ndoa yao.

8: Wanandoa hawawezi kutatua mgogoro wowote uliopo kati yao endapo mwanaume atakuwa na mchepuko. Hii ni kwa sababu mke anakuwa na kinyongo kwakuwa mumewe ana uhusiano wa kimapenzi na mwanamke mwingine, na mwanaume anakuwa na wasiwasi wa kuongea na mkewe kwa sababu ya kuhofia kuwa mazungumzo hayo yanaweza kuibua uhusiano wake na mchepuko. Hivyo, matatizo kwenye ndoa yanabaki kutotatuliwa kwakuwa wanandoa wenyewe hawapati muda wa kuyazungumza na kutafuta suluhu.

9: Mara nyingine kuwa na mchepuko husaidia kutatua matatizo ya ndoa. Je, michepuko ndio chanzo cha kuvunjika kwa ndoa? Si mara zote. Kwakuwa uhusiano mpya unakuwa na hamasa kubwa, mchepuko unaweza kusaidia kuamsha hisisa za mapenzi yenu. Mwanaume hujua nani anayemtaka maishani mwake na kwamba uhusiano alioanzisha na mchepuko hauna utulivu kama alivyotarajia. Kama ilikuwa ni kujisahau kwa mara moja tu basi ni rahisi kwa mwanaume huyu kurudi kwa mkewe.

10: Mke si wa kulaumiwa kwa mumewe kuwa na mchepuko. Zingatia mfano ufuatao: kama mumeo ana mchepuko, hili si kosa lako, haijalishi watu watakwambia nini. Mwanaume anapochepuka ujue ameamua mwenyewe kufanya hivyo. Mawazo kwamba ameshawishika au ameteleza na kujikuta amefanya mapenzi na mchepuko si kweli kabisa. Mwanaume hachepuki kwa sababu ya vitu atakavyovipata kwa mwanamke mwingine, anachepuka kwa kufikiria vitu anavyovikosa kwa mwanamke wake. Lawama zinaibuka kwa sababu ya wawili hao kudharau matatizo waliyonayo na kutoyatafutia suluhu.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad