Maombi ya Musukuma kwa Rais Magufuli leo


Mbunge wa Geita Joseph Kasheku (Musukuma) amedai kuwa wananchi wake wamempa ubunge wa kudumu katika jimbo lake na kuongeza kuwa kwa sasa jimbo lake ndilo lenye barabara nzuri kuliko Geita nzima licha ya kutokuwa na lami.

Aidha 'amejifagilia' kwa kuwezesha maendeleo makubwa Jimbo lake na kumuomba Rais Magufuli iwapo itampendeza kuwapatia shilingi milioni 200 itakayowezesha ujenzi wa hospitali itakayozidi kwa ubora wa vifaa hata Hospitali ya Bugando baada ya kupokea msaada wa vifaa vya kisasa kutoka kwa wafadhili na wamiliki wa mabasi.

Musukuma pia ameendelea na kilio chake cha kupatiwa maaskari wa kike na kuongeza kwamba uhalifu wa kukatana mapanga umepungua.

“Mh.Rais, Polisi ni marafiki zangu sana siwashtaki, Jimbo langu lilikuwa linaongoza kwa wakata mapanga, tukajitoa tukajenga kituo, sasa hakuna wakata mapanga shida yangu ni moja tu, jimbo zima hakuna askari wa kike, lakini nikiomba askari wa kike naambiwa kuna mgao”.

Aliendelea kwa kusema, "Mh.Rais ikukupendeza nisaidie nipewe hata askari wanne wa kike kwenye Jimbo langu hakuna askari wa kike hata mmoja, wanawake wapo kwenye mazingira magumu, wanakaguliwa na askari wa kiume na mnajua maumbile ya wasukuma yalivyo,".

Ikafika wakati kwa Rais Magufuli kujibu maombi hayo ambapo alieleza, "IGP vijana wako wa Polisi wanapigaga nyimbo nzuri lakini nimeshangaa hata viuno wanajua kukatika nilifikiri mmekodisha, hongereni mazoezi yote mnayajua, mmeiva katika mambo yote, inawezekana ndio sababu Mh.Msukuma ameomba askari wa kike, IGP usimnyime mchagulie waende uko".

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad