Marekani yaidhinisha uuzaji wa silaha kwa Taiwan licha ya China kupinga mpango huo

Idara ya maswala ya kigeni nchini Marekani imeidhinbisha uuzaji wa silaha kwa Taiwan , utakaogharimu $2.2bn (£1.76bn), Pentagon imesema.

Mpango huo ni wa vifaru 108 , makombora 250 na vifaa vinavyohusiana.Mwezi uliopita , wixzara ya maswala ya kigeni nchini China iliitaka Marekani kusitisha uuzaji huo , ukiutaja kuwa swala nyeti na uamuzi mbaya.

China unaichukulia eneo la Taiwan kuwa miongoni mwa himaya yake ambayo inafaa kuunganishwa na nchi kavu kwa nguvu iwapo zitahitajika.

Ndege iliyotengenezwa na wanafunzi yafika Misri

Msemaji wa wizara ya maswala ya kigeni geng Shuang pia aliitaka Marekani kuheshimu sera ya China ya taifa moja ambapo marekani inatambua China na sio Taiwan.

Uuzaji wa silaha hizo hautaathiri uwezo wowote wa kijeshi katika eneo hilo , ilisema marekani. Idara ya ulinzi tayari imelieleza bunge kuhusu uuzaji huo wa silaha.


Afisi ya rais wa Taiwan imeelezea furaha yake kwa Marekani ambayo ndilo taifa linalouzia taiwan silaha.

Msemaji wa rais wa taiwan alisema katika taarifa kwa reuters kwamba kisiwa hicho kitendelea kuimarisha uhusiano wake ewa kiusalama na Marekani

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad