Marekani Yatuma Wanajeshi 500 na Silaha nzito za Kivita Nchini Saudi Arabia, Muda Wowote Iran inashambuliwa
0
July 21, 2019
Marekani imetuma wanajeshi wapatao 500 na silaha nzito za kivita kwenda nchini Saudi Arabia kuweka kambi, Hii ni kufuatia vugu vugu lake na Iran.
Kwa mujibu wa kituo cha runinga cha kimataifa cha CNN, Kimesema kuwa wanajeshi hao huenda wameshapelekwa kimya kimya wiki iliyopita na hii inakuwa ni mara ya pili Marekani kufanya hivyo tangu mwaka 2003 ilipopeleka wanajeshi 1000 katika uwanja wa ndege za kivita wa Prince Sultan mjini Al Kharj nchini Saudi Arabia.
Mgogoro kati ya Iran na Marekani ni wa muda mrefu ukihusiana na masuala ya utengenezaji wa silaha za nyuklia jambo ambalo Iran imekuwa ikikanusha na kueleza kuwa inatengeneza kwa malengo ya kujilinda na sio vinginevyo.
Uhusiano wa Iran na Marekani umezidi kudhoofika mwaka huu, Ambapo mwezi May zaidi ya meli 5 zilizokuwa zimebeba mafuta na kukatiza katika mlango wa bahari wa Hormuz, Zilikamatwa na Iran bila ya maelezo ya kina.
Baadae mwezi Juni mwaka huu, Ndege isiyokuwa na rubani iliyotumwa na Marekani katika maeneo ya bahari ya Hormuz ilitunguliwa na Iran, Huku Marekani ikithibitisha taarifa hizo kwa uchungu.
Wakati hayo yakiendelea, Wiki iliyopita Iran tena imeizuia Meli kubwa ya mafuta ya Uingereza kwa sababu iliyoleza kuwa ilikuwa na mafuta ya magendo.
Kwenye Meli hiyo watu 12 tayari wameshakamatwa na serikali ya Iran, huku mataifa ya Ufaransa, Marekani na Ujerumani yakiitaka Iran iiachilie Meli hiyo kabla ya mambo hayajawa mabaya.
Tags