MAOFISA wa Marekani na Israel wamesema wamefanikiwa kufanya majaribio ya makombora ya ulinzi huko Alaska, Marekani.
Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, alisema Jumapili (jana) wamefanya majaribio ya makombora aina ya Arrow-3 ambayo yameipa nchi yake uwezo wa kudhibiti makombora makali yanayofyatuliwa kutoka Iran na maeneo mengine
Wizara ya ulinzi ya Marekani imesema kombora hilo lina uwezo wa kufikia umbali mrefu na Netanyahu alisema ufanyaji kazi wa makombora hayo ni mzuri.
“Maadui zetu wafahamu kwamba tunaweza kukabiliana nao, kwa njia zote za ulinzi na mapigano,” alisisitiza.
Idara zinazohusika na makombora ya ulinzi ya Marekani na Israel zilipanga kufanya jaribio la kwanza la kombora hilo kwenye anga ya Alaska katikati ya mwaka 2018 lakini waliahirisha wakisema kuwa walihitaji kuboresha zaidi mfumo huo.