Siku chache baada ya Watanzania 9 kuuawa mkoani Mtwara, mpakani mwa Tanzania na Msumbiji IGP Simon Sirro na IGP wa Msumbiji Bernardino Rafael, wamekutana ili kupanga namna ya kuwanasa watuhumiwa na tukio hilo.
Makubaliano baina ya IGP Sirro na IGP Bernardino Rafael yamefikiwa mkoani Mtwara ambapo wamekubaliana kila mmoja, kuweka mbali suala la mipaka ya nchi zao, kwenye kupambana na uhalifu baina ya nchi hizo mbili.
"Tumeweka mikakati ya pamoja kupambana na hao wahalifu wanaosumbua Watanzania na Wasumbiji kuwa hawana mipaka, kwa hiyo na sisi mipaka isitufanye tukashindwa kupambana na uhalifu, na tumekubaliana wale waliofanya mauaji ya watu 9 watafutwe kila kona ili kuchukuliwa hatua za kisheria." amesema IGP Sirro
"Ukimuua Mtanzania popote ulipo ujue, haupo salama ila niwaombe pia Watanzania popote ulipo ukitaka kwenda Msumbiji uende kwa tahadhari sana." amesema
Julai 29, akiwa mkoani Mtwara IGP Simon Sirro alitangaza kuuawa kwa Watanzania 9, waliokwenda nchini Msumbuji kwa ajili ya kujitafutia kipato.
Mauaji ya Watanzania 9 Yawakutanisha IGP Sirro na IGP wa Msumbiji ili Kupanga Namna ya Kuwanasa Watuhumiwa
0
July 01, 2019
Tags