Mbunge Heche"Serikali inatakiwa kupambana na uchumi na sio kuwapiga wananchi mabomu"



Mbunge wa Tarime Vijijini (Chadema), John Heche amesema serikali badala ya kupambana kuongeza uchumi wanatumia nguvu kubwa na gharama kupambana na upinzani.

Heche aliayasema hayo kupitia ukurasa wake wa Twitter kuwa serikali badala ya kupambana kuongeza watalii matokeo yake inatumia nguvu kubwa kupambana na wananchi.

Alisema mwanamke ambaye amezimia kwa kupigwa bomu katika kikao cha ndani cha Bariadi ni jambo la aibu.

Mbunge huyo aliandika ujumbe huu”Mwanamke ambae amezimia kutokana na kupigwa mabomu kwenye kikao cha ndani Bariadi Simiyu. Serikali hii badala ya kupambana na kuleta watalii kuongeza uchumi wanatumia nguvu na gharama kupambana na upinzani. Shame,” alieleza.

Jana Jeshi la polisi lilivamia mkutano wa Baraza la wanawake wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (BAVICHA) na kuwapiga mabomu ya machozi.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad