Mbunge Lema "Ni Bora Kufutwa Mfumo wa Vyama Vingi Kuliko Jeshi Kuingia Katika Siasa"


Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema amesema ni bora kufuta mfumo wa vyama vingi kuliko kuliingiza jeshi katika masula ya siasa ni kusababisha machafuko.

Lema ameyasema hayo leo kupitia ukurasa wake wa kijamii wa Twitter, alidai kuwa kauli ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha katika mkutano wa Chama cha Mapinduzi hivi karibuni alitoa kauli mbaya inayolenga mpasuko katika jamii.

Amesema kuliingiza jeshi katika siasa ni kuleta machafuko katika jamii.

Lema aliandika hivi”Kwa vile hakuna ujinga unaoshindikana kwa sasa, ni bora kufuta mfumo wa vyama vingi kuliko kuliingiza jeshi la polisi katika siasa. Kauli ya RPC Arusha katika mkutano wa CCM hivi karibuni ni kauli mbaya inayoleta mpasuko katika jamii. Kuliingiza jeshi katika siasa ni kuleta machafuko katika jamii,”

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad