Mbunge wa jimbo la Iramba Magharibi, Mwigulu Nchemba amemtaka kiongozi wa ACT Wazalendo, Zitto Kabwe kutambua Rais John Magufuli ametekeleza ilani kwa kiwango cha juu.
Nchemba ambaye alishawahi kuwa Waziri wa Mambo ya Nchi aliandika ujumbe huo kupitia ukurasa wake wa kijamii wa Twitter akimtaka Zitto kutambua mafanikio ambayo ameyafanya Rais Magufuli.
Aliandika ujumbe unaosomeka hivi”Bwana Zitto elewa Rais Magufuli ametekeleza ilani kwa kiwango cha juu sana umeme zaidi ya vijiji 7,100 mpaka sasa na kazi inaendelea, lami imefungua mikoa ya Singida, Tabora, Simiyu na sasa mpaka Kigoma usikoona,”
Bwana ZITTO, elewa, Rais MAGUFULI ametekeleza Ilani kwa kiwango cha juu Sana, Umeme zaidi ya Vijiji 7,100 mpaka sasa na kazi inaendelea, Hospitali zaidi ya Tarafa 350 na Kazi inaendelea, Lami imefungua mikoa ya Singida, Tabora, simiyu, na sasa mpaka Kigoma usikoona pic.twitter.com/Amg8Qe5kD1
— Dr.Mwigulu Nchemba (MG) (@mwigulunchemba1) July 29, 2019
2.Maji zaidi ya asilimia za kwenye ilani, Mabweni Kazi inaendelea. Haya Ni ya jamii tu, Njoo miradi ya Kihistoria, kama SGR, Nyerere power Station ya Rufiji, Ndege, Vivuko, Meli na Madaraja ambavyo hata usipovisemea vizuri wewe, Watoto wako na wajukuu watakuja kusema kuwa.. pic.twitter.com/XBOjX9hoPe
— Dr.Mwigulu Nchemba (MG) (@mwigulunchemba1) July 29, 2019