Mjukuu wa Nyerere: Nimeshuhudia Babu Akitaa Sanamu Tatu Mbele Yangu


Mjukuu wa Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Sophia Nyerere amekosoa sanamu ya Mwalimu Nyerere iliyozinduliwa wakati wa halfla ya uzinduzi wa Hifadhi mpya ya Wanyamapori ya Burigi iliyopo wilayani Chato mkoani geita na kudai kwamba laiti kama angekuwepo basi angekataa sanamu hiyo.

Katika hafla hiyo iliyofanyika Julai 9, Rais John Magufuli ndiyo aliyekabidhiwa kuzindua sanamu hiyo na Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla ambapo inaashiria ujumbe maalum kuhusu umuhimu wa utunzaji wa mazingira ya wanyamapori.

Sophia Nyerere amesema kwamba wakati akiwa mdogo kiasi mwishoni mwa mwaka 1998 na mwanzoni mwaka mwa mwaka 1999 mwanzoni kabla ya kifo chake Oktoba 14 mwaka 1999 amewahi kumshuhudia babu yake akikataa sanamu tatu ambazo aliletewa

Yafuatayo chini ndiyo maelezo yake;

“Napenda kuwapongeza viongozi wa nchi ikiwemo Mheshimiwa Rais Dr. John Joseph Pombe Magufuli na Mheshimiwa Hamisi Kigwangala kwa kazi nzuri. Ningependa kutoa shukrani za dhati kwa hatua hii kubwa ya kumuenzi baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kwa vitendo.”

Napenda kuwapongeza viongozi wa nchi ikiwemo Mheshimiwa Rais Dr. John Joseph Pombe Magufuli na Mheshimiwa Hamisi Kigwangala kwa kazi nzuri. Ningependa kutoa shukrani za dhati kwa hatua hii kubwa ya kumuenzi baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kwa vitendo. Ningependa pia kutoa ufafanuzi kidogo kuhusiana na baba wa Taifa Mwalimu J.k.Nyerere ambae alikuwa ni babu yetu. Nikiwa kama mjukuu namkumbuka babu kwa mengi sana. Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alipokuwa hai miaka ya 1998 na 1999 mwanzoni kabla ya kifo chake 14.10.1999 aliwahi kuletewa sanamu tatu na zote alizikataa. Nilishuhudia hili kwa macho yangu mbele ya brigedia Orasa ambae alikuwa akisimamia ujenzi wa nyumba yake ya Mwitongo. Alipinga sana sanamu hizi ambazo haziendani na sura yake .. Mimi ni shahidi @drjohnpombemagufuli babu alikubali Ile sanamu iliopo Mwitongo pale nyumbani karibu na kaburi lake. Sanamu Ile alikubali baada ya kijiridhisha .Mimi binafsi kwa akili timamu nakumbuka siku hiyo wageni walikuja na hizo sanamu baada ya kuondoka nyumbani babu hakurudi tena nyumba ya zamani tukaenda nyumba mpya ambapo ndio kaburi lake lilipo. Baada ya kuzunguka na mazungumzo yake na brigedia Orasa wakati huo alikuwa kanali tulienda pale ilipo sanamu yake sasa, wakati huo kulikuwa na migomba na kuna mchina Mr Lee akiwepo akisimamia bustani yake nakumbuka babu alinishika mkono kwa utani akiniuliza eti dada yangu "nafanana na hiyo sanamu"? Nikajibu, ndio nakumbuka alinigusa kichwani akiniangalia machoni akaniuliza mimi nafanana na sanamu nikwambia unafanana nayo akacheka akasema nitafananaje na sanamu wakati nipo hai? Mwisho akasema haya iacheni hapo tukaondoka kurudi nyumba ya zamani.. Mimi nimelelewa katika misingi ya maadili natambuwa kuwa hata mtoto uliemzaa mwenyewe akishakuwa kiongozi unapaswa kumheshimu hiyo mheshimiwa Raisi na waziri hatuwezi kuwapangia wafanye nini maana itakuwa sio sahihi ni wenyewe tu wakikumbuka kuwa Azimio la Arusha ndio lilibeba roho ya Mwalimu basi na sanamu hiyo ingekuwa vyema iendane nae na sisi familia na wa Tanzania tatafurahi kuona sura halisi ya Baba wa Taifa kama Mwenyewe alivyokuwa akipenda muonekano wake udumishwe. 🙏

“Ningependa pia kutoa ufafanuzi kidogo kuhusiana na baba wa Taifa Mwalimu J.k.Nyerere ambae alikuwa ni babu yetu. Nikiwa kama mjukuu namkumbuka babu kwa mengi sana. Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alipokuwa hai miaka ya 1998 na 1999 mwanzoni kabla ya kifo chake 14.10.1999 aliwahi kuletewa sanamu tatu na zote alizikataa. Nilishuhudia hili kwa macho yangu mbele ya brigedia Orasa ambae alikuwa akisimamia ujenzi wa nyumba yake ya Mwitongo. Alipinga sana sanamu hizi ambazo haziendani na sura yake.”

“Mimi ni shahidi @drjohnpombemagufuli babu alikubali Ile sanamu iliopo Mwitongo pale nyumbani karibu na kaburi lake. Sanamu Ile alikubali baada ya kijiridhisha. Mimi binafsi kwa akili timamu nakumbuka siku hiyo wageni walikuja na hizo sanamu baada ya kuondoka nyumbani babu hakurudi tena nyumba ya zamani tukaenda nyumba mpya ambapo ndio kaburi lake lilipo.”

“Baada ya kuzunguka na mazungumzo yake na brigedia Orasa wakati huo alikuwa kanali tulienda pale ilipo sanamu yake sasa, wakati huo kulikuwa na migomba na kuna mchina Mr Lee akiwepo akisimamia bustani yake nakumbuka babu alinishika mkono kwa utani akiniuliza eti dada yangu “nafanana na hiyo sanamu”? Nikajibu, ndio nakumbuka alinigusa kichwani akiniangalia machoni akaniuliza mimi nafanana na sanamu nikwambia unafanana nayo akacheka akasema nitafananaje na sanamu wakati nipo hai? Mwisho akasema haya iacheni hapo tukaondoka kurudi nyumba ya zamani.”

“Mimi nimelelewa katika misingi ya maadili natambuwa kuwa hata mtoto uliemzaa mwenyewe akishakuwa kiongozi unapaswa kumheshimu hiyo mheshimiwa Raisi na waziri hatuwezi kuwapangia wafanye nini maana itakuwa sio sahihi ni wenyewe tu wakikumbuka kuwa Azimio la Arusha ndio lilibeba roho ya Mwalimu basi na sanamu hiyo ingekuwa vyema iendane nae na sisi familia na wa Tanzania tatafurahi kuona sura halisi ya Baba wa Taifa kama Mwenyewe alivyokuwa akipenda muonekano wake udumishwe.”

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad