Mo Dewji Afunguka Kuhusu Simba ”Waziri Alituruhusu Tuendelee na Mwekezaji Mmoja, Mimi Nipo na Niko na Nyinyi, Siendi Popote”



Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya klabu ya Simba, Mohammed Dewji ameonyeshwa kusikitishwa na mijadala kwamba ameanzisha utaratibu mpya ya uwekezaji badala ya ule ulipangwa na Serikali.

Kupitia akaunti yake ya kijamii ya Instagram, Mo ameandika kuwa habari hizo si zakweli bali utaratibu huo wa mwekezaji kuwa na 49% na wanachama 51% ya hisa upo kisheria na wao kama Simba waliukubali.

”Nimesikitishwa na mijadala mitandaoni ya kumshutumu Waziri Mwakyembe kwamba ameanzisha utaratibu mpya wa mwekezaji kuwa na 49% na wanachama 51% ya hisa. Ndugu zangu, si kweli. Utaratibu huu upo tangu 2017 kisheria na sisi Simba tulikubali.”- Ameandika Mo Dewji.

Mfadhili huyo wa Simba, Mohammed Dewji  ameongeza kuwa

 ”Waziri Mwakyembe alituruhusu SIMBA tuendelee na mwekezaji mmoja. Ndugu WanaSimba Mimi nipo na niko na nyinyi, siendi popote.”
”Na sasa tumeishazungumza na Serekali na mazungumzo ni mazuri. Nawasihi WanaSimba wote twendeni tukaishangilie Timu ya Taifa na tukutane Simba Day tarehe 6. Tulianza vizuri na Serikali na tutamaliza vizuri na Serikali.”

Siku za hivi karibuni kumekuwa na mijadala mbalimbali juu mfumo wa uwekezaji wa klabu ya Simba wa mfadhili kuwa na hisa 49% na wanachama 51% huku kukigubikwa na wingu la swala la baraza la wadhamini ambalo miamba hiyo ya soka ya Karia Koo ilijaribu kuliweka sawa wiki iliyopita baada ya kufanya mkutano wake na waandishi wa habari jijini Dar Es Salaam.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad