Moni Centrozone 'Sitaki Kabisa Mpenzi Wangu Nai Awe na Urafiki na Tunda"


Mkali wa Rap bongo, Moni Centrozone amempiga marufuku mpenzi wake Nai kuwa karibu na mwanadada maarufu mtandaoni, Tunda ikiwemo kuhudhuria sherehe zake na sehemu za starehe.

Akipiga stori na eNewz ya EATV, Moni amesema kuwa ameamua kufanya hivyo kutokana na kwamba Tunda si mhudhuriaji mzuri wa shughuli za Nai kwahiyo hakuona umuhimu wa yeye kumruhusu kwenda kwenye siku ya kumbukizi yake ya kuzaliwa iliyofanyika hivi karibuni.

"Mimi hata zamani mama alikuwa akiniuliza sana kuwa ninakwenda kwa marafiki zangu tu lakini rafiki zangu hawafiki nyumbani, kwahiyo hata Nai nimemwambia 'mama tulia' hao hata tukiwa tunazindua kitu chetu hawatokei", amesema Moni.

"Sipendezwi kuona mpenzi wangu anaishi maisha ya kustarehe tu, sisi ni watu wa kazi tunatafuta pesa, ndiyo maana unaona tunapiga show, tunafungua maofisi na kila kitu. Sipendi maisha hayo ya Tunda ya kustarehe tu", ameongeza.

Mtazame Moni Centrozone akifunguka zaidi hapa chini

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad