Mpango wa FIFA na CAF kuwasilishwa mahakamani


Mpango wa shirikisho la kandanda duniani (FIFA) kuchukua mikoba ya uendeshwaji wa kandanda la Afrika unatarajiwa kukumbwa na kizuizi.

Hii ni kutokana na mwanachama mmoja wa kamati kuu ya shirikisho la soka Aftika (CAF) Hasan Bility toka Liberia amesema ataiomba mahakama ya upatanishi ya michezo yenye makao makuu yake nchini Uswisi kutangaza kuwa makubaliano hayo ni batili ambayo katibu mkuu wa FIFA Fatma Samoura atatumwa kwenda kulifanyia mageuzi shirikisho la soka Afrika (CAF).

CAF ipo katikati ya mgogoro kufuatia tuhuma za rushwa dhidi ya rais wa shirikisho hilo Ahmad ambazo anakanusha. FIFA imesema haina cha kuongezea kwa muongozo wa mpango wa kulisaidia kandanda la Afrika.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad