Msanii Jay Z ageukia biashara ya bangi

Mwanamuziki kutokea Marekani, Shawn Carter maarufu kama Jay Z Jay Z inadaiwa yupo mbioni kuingia makubaliano yakibiashara na kampuni ya California Cannabis Product ambayo ndio wazalishaji na wasabambazaji wa bangi katika nchi zilizohalalisha matumizi ya bangi ikiwa ni mpango wake wakuendelea kuwekeza ili aweze kutengeneza fedha zaidi.

Kwa mujibu wa mtandao wa Culture umeripoti kuwa msanii huyo anataka kutengeneza ajira nyingi zaidi kadri awezavyo ili jamii yake iweze kujinasua kutoka kwenye hali ngumu yakimaisha.

Ikumbukwe mapema mwezi Juni mwaka huu, Jay Z alitajwa na Jarida la Forbs kama msanii wa kwanza wa Hip Hop kuwa Bilionea, akiwa na utajiri wa $1 Bilioni (sawa na Tsh. Trilioni 2.2).

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad