Msekwa Afunguka Kuhusu Barua ya Makamba na Kinana Kudai Kudhalilishwa na Cyprian Musiba


Katibu wa baraza la ushauri la viongozi wastaafu CCM, Pius Msekwa amesema malalamiko ya makatibu wakuu wawili wa chama hicho atayapeleka ngazi za juu kwa hatua zaidi.

Juzi, makatibu wakuu hao wawili wastaafu wa CCM, Yusuf Makamba na Abdulrahman Kinana, walimwandikia barua Msekwa wakilalamika kudhalilishwa kwa mambo ya uongo na mtu anayejitambulisha kama mwanaharakati na mtetezi wa Serikali.

Msekwa ambaye alisema barua hiyo ambayo ni ya kwanza kuwafikia wao kama Baraza la Wazee Wastaafu, kwa kawaida itapelekwa kwenye chama hicho ambacho ndicho kinachopaswa kuitisha vikao kushughulikia malalamiko yaliyotajwa.

Amesema nakala nyingine za barua hiyo zimepelekwa kwa Mwenyekiti wa CCM, Rais Magufuli na Katibu Mkuu, Dk. Bashiru Ally.

“Hii ni mara ya kwanza kupokea malalamiko ya aina hii, kwanza hakuna utaratibu wa kawaida, lakini tutafuata taratibu za chama, tutapeleka kwenye chama chenyewe." Amesema na kuongeza;

“Barua hii nakala yake imeenda pia kwa Mwenyekiti wa chama na Katibu Mkuu"

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Mzee mmwenzangu Msekwa.
    Kwa busara za kibinaadamu na uStaarabu wetu ni vyema kkuonesha kuwa umeipokea na iko pending for evaluation / under evaluation.

    sababu ziko wazi na ukweli tunaujua na haufichiki.
    Musiba yuko Sahihi kwa muono wake na walio wenngi. na Uhuru huo anao..!!
    kwa nini hakukuingilia wewe mzee Ruksa m7ngu ampee umui au Salim Ahmed Salim Ajilihamna uchu na uanishaji magenge haya yalibainka vizuri katika khakiki Mali za Chama Hata Dkt Bashiru natimu yetu tunayajua fika. Acha kkawa liiendelee kuunika mtungi na mwana harakati aaendele na harakati bila bugudha anaetaka ajibu mapigo au anyamaze uhuru na uwanja ni wake angali Mkapa kakaa kwa Tahadhari angalia Lowassa kaamua kurudi nyumbani

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad