Mahakama ya Kenya imemhukumu Mtanzania Rashid Mberesero kifungo cha maisha jela baada ya kumkuta na hatia ya kutekeleza shambulio la kigaidi mwaka 2015 katika Chuo Kikuu cha Garissa, Kenya.
Rashid Mberesero amehukumiwa kutumikia adhabu hiyo, akiungana na watu wengine wawili ambao kwa pamoja wamekutwa na hatia ya kuhusika na shambulio la kigaidi lililosababisha vifo vya wanafunzi 148 katika chuo hicho.
Wakati Rashid Mberesero akihukumiwa adhabu ya kifungo cha maisha jela, washtakiwa wenzake wawili Hassan Edin na Mohammed Abdi jina jingine Mohamned Ali Abikar wamehukumiwa miaka 41 kila mmoja gerezani.
Rashid Mberesero, aligundulika katika eneo la tukio akiwa sio mwanafunzi wala mfanyakazi wa chuo hicho.
Gazeti la The Citizen Tanzania la Aprili 10 mwaka 2016, lilisema Rashid alikuwa akisoma shule ya upili ya Bihawana mjini Dodoma Tanzania ambaye alidaiwa kutoroka shule baada ya kukatazwa kuvaa kofia kichwani.
Kulingana na mwalimu mkuu wa shule hiyo wakati huo, mwanafunzi huyo alijiunga na shule hiyo mwaka 2015 baada ya kutoka shule ya upili ya Bahi Kagwe.
Licha ya kutoweka katika shule, hakuna aliyefuatilia alikokwenda
Kwa takriban miezi minne wazazi wa kijana huyo walidhani mtoto wao yupo shule lakini haikuwa hivyo.
Haijulikani ni nini haswa kilichomfanya kuingia katika ugaidi.
Wazazi wa Rashid walishangaa kugundua kwamba mtoto wao alikuwa miongoni mwa watu waliopanga na kutekeleza shambulio la Garissa
Mtanzania Ahukumiwa Maisha Kenya Kwa Kuhusukika na Shambulizi la Kigaidi Lililoua Watu 148
0
July 04, 2019
Tags