Stephan E, mtuhumiwa mkuu katika mauaji ya mwanasiasa wa Ujerumani Walter Luebke Juni 2, amebadilisha hatua yake ya awali ya kukiri kosa jana, kwa mujibu wa wakili wake.
Wiki iliyopita, Stephan E, alikiri kumuua Luebke, mwanasiasa wa jimbo, nyumbani kwake karibi na Kassel, Ujerumani. Katika tamko lake la awali la kukiri, mshitakiwa alidai alikuwa peke yake katika mauaji hayo, ambapo wachunguzi katika kesi hiyo wanasema hiyo haiwezekani.
Wachunguzi wanashuku kwamba kubadilika huko huenda ni mbinu zake. Stephan E, ana rekodi ya uhalifu na anafahamika kuhusika katika kundi la watu wenye misimamo mikali ya mrengo wa kulia.
Kabla ya kuuwawa, Luebke alipokea vitisho kadhaa vya kumuua kwa kuunga mkono sera ya kansela Angela Merkel ya kufungua milango kwa wakimbizi.
Mtuhumiwa wa Mauaji Abadilisha Maelezo Yake ya Kukiri Kosa
0
July 03, 2019
Tags